Kiungo wa Arsenal ambaye alizua wasi wasi mkubwa wa kuondoka klabuni
hapo mwishoni mwa msimu huu, Mesut Ozil amesaini mkataba mpya wa
kuendelea kuchezea timu hiyo kwa miaka mitatu na nusu ijayo.
![]() |
| Mesut Ozil akisaini mkataba wake wa kuendelea kubakia Arsenal huku kushoto akiwa amesimamiwa na kocha Arsene Wenger. |
Ozil ambaye mkataba wake ulikuwa unafikia tamati mwisho wa msimu huu,
amesaini mkataba huo ambapo atakuwa analipwa mshahara wa kiasi cha
paundi 300,000 kwa wiki ikiwa ni tofauti ya paundi 120,000 kati ya
mshahara wake na ule anaulipwa Pierre-Emerick Aubameyang aliyesajiliwa
wiki hii katika timu hiyo.
Mesut ameonekana mwenye furaha kubwa baada ya kusaini mkataba huo,
kutokana na ujumbe ambao ameuandika katika mitandao yake ya kijamii.
“#YaGunnersYa …. ooh yaaa Proud to announce: I signed dat thing
3 more years with @Arsenal! It’s been one of the most important
decisions of my footballing career and that’s why I had to think hard
and talk with everyone who’s important to me,” ameandika Ozil.
“Good things take time! In the end I let my heart decide. As I always
said, I feel at home here and I’m highly motivated to achieve big
things in the next few years. Once a Gunner, always a Gunner! #M1Ö #WeAreTheArsenal #London,” ameongeza.
Kutokana na hatua hiyo, kwa sasa Ozil atakuwa mchezaji wa pili
anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika ligi kuu ya Uingereza akiongozwa
na Alexis Sanchez wa Manchester United ambaye analipwa paundi 350,000
kwa wiki.


0 comments :
Post a Comment