Mchezaji tennis namba moja nchini Uingereza, Johanna Konta amesema kuwa
majira haya ya joto atakuwa na ratiba ngumu zaidi kuelekea michuano ya
Wimbledon.
Konta ameyasema hayo kufuatia kuingia katika mashindano matatu kwa
mpigo ambayo ni Nottingham Open, Birmingham Classic na Eastbourne
International yatakayo muwezesha kuwafiti wakati wa michuano yaWimbledon.
Johanna Konta mwenye umri wa miaka 26, mwaka jana alishindwa kufanya
vizuri katika michuano hiyo ya Nottingham Open hata hivyo alifanikiwa
kuwa mwanadada wa kwanza wa Uingereza kufika hatua ya nusu fainali ya
Wimbledon kwa mchezaji mmoja mmoja tangu alivyoweza kufanya hivyo
Virginia Wade mwaka1979.
“Huu ni moja kati ya msimu niupendao na hakuna wa kuufananisha hasa
mashindano yakiwa nyumbani ambapo kuna mashabiki, marafiki na familia
ikiwa nyuma yako inakushabikia,”amesema Konta kupitia chombo cha habari
cha Skysport.

0 comments :
Post a Comment