Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ya klabu ya Simba, Haji Manara
kupitia mkutano wake na waandishi wa habari mchana wa leo amesema kuwa
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili.
Alhaj Ali Hassan Mwinyi anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya timu
Gendarmerie Nationale FC siku ya Jumapili.
Kwenye mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa makao makuu ya Simba
SC, Manara amesema “Tunategemea kuwa Mzee wetu, Rais mstaafu wa Awamu
ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuwa mgeni rasmi wa mchezo wetu dhidi
ya Gendarmerie Nationale FC kwenye michuano ya kombe la shirikisho la
CAF , mchezo huu ambao utachezwa Jumapili saa 10:00 jioni katika uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam,” amesema Manara.
Kikosi cha Gendarmerie Nationale FC kinatarajiwa kuwasili siku ya
Jumamosi majira ya saa 7:00 usiku kikitokea Djibouti kikiwa ni msafara
wa watu 18 na viongozi nane.
Viingilio vya mchezo huo vitakuwa ni 30,000 kwa VIP A, 20,000 VIP B, Orange 10,000 na 5,000 kwa mzunguko.

0 comments :
Post a Comment