Mara baada ya kutokea purukushani uwanjani ambapo ilimfanya mchezaji
Mau Bofu kupewa kadi nyekundu na kutolewa nje katika mchezo dhidi ya
Simba, kuna habari kuhusu kilichotokea.
Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ambaye ni mkongwe katika
cheo hicho, ameomba radhi kwa niaba ya mchezaji wake, Mau Bofu kwa tukio
hilo akisema ni kweli alifanya makosa na anastahili kusamehewa.
Bwire amesema mchezo wa soka ni mchezo wa kugusana, sasa inapotokea
mmoja amemgusa mwenzie mpaka amepitiliza au amezidi kiwango
kinachotakiwa ni jambo la kawaida kuona adhabu ikitolewa kwa mhusika.
Ofisa huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu amesema kuwa Bofu hakuwa na
nia ya kumuumiza Okwi na ndiyo maana ametambua kosa lake, hivyo anaomba
msamaha kwa Wnasimba, wadau wa soka na kwa Okwi mwenyewe ambaye ndiye
aliyejeruhiwa.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Bofu alimpiga kwa makusudi
Okwi sehemu ya shingo na kusababisha mchezaji huyo kushindwa kuendelea
na mchezo huku Bofu akitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Simba ilishinda mabao 3-0 katika kipute hicho kilichopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

0 comments :
Post a Comment