BODI YA LIGI NA TFF KUAMUA NANI ACHEZE LIGI KUU MSIMU WA 2018/2019.

Bodi ya Ligi (TPLB) pamoja na Shirikisho la Soka nchini (TFF) imesema inasubiri kamati ya saa 72 baada ya mechi za Ligi daraja la kwanza FDL kukamilika ili kutangaza timu sita zilizopanda rasmi kushiriki Ligi kuu msimu ujao. 


Mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema, ni kanuni ndizo zinazoelekeza kwamba ndani ya saa 72 baada ya mechi zote kumalizika timu zinanafasi ya kupeleka malalamiko yoyote kama yapo. 

"Kwahiyo sisi kikanuni tutatangaza timu zilizopanda rasmi mara baada ya saa 72 kutimia,  " amesema. 

Wambura amesema mpaka sasa hawajapokea malalamiko yoyote kutoka kwenye timu za FDL hivyo wanaendelea kusubiri kama kanuni inavyosema.
Share on Google Plus

About Tiktak

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment