Bondia Muhammad Ali, raia wa
uingereza amefungiwa kwa miaka miwili kujihusisha na mchezo wa masubwi
baada ya kushindwa vipimo vya dawa zilizokatazwa michezoni.
Ali
mwenye miaka 21, alishindwa kufaulu vipimo alipokua nashikiriki michezo
ya dunia ya masubwi iliyofanyika nchini Morocco mwaka jana.
Bondia
huyo alisimamishwa toka mwezi octoba mwaka jana na amefikia makubaliano
ya kukubali adhabu hiyo na chama cha kimataifa cha mchezo wa ndondi.
(AIBA).
Vipimo vinaonyesha bondia huyu amekuwa akitumia dawa aina
ya Trenbolone, ambazo hutumika kukuza na kusisimua misuli na dawa hizo
zimekatazwa michezoni na Wada.

0 comments :
Post a Comment