Mkufunzi wa Manchester City Pep
Guardiola amekataa kumlaumu Raheem Sterling kwa mkosi wa kikosi chake
kushindwa kuilaza Burnley baada ya mshambuliaji huyo wa Uingereza kukosa
nafasi ya pekee.
Huku ikiwa 1-0 na dakika 20 chini ya ushindi wao
wa 23 msimu huu, Sterling alishindwa kucheka na wavu akiwa maguu sita
baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Kyle Walker.
Kisa hicho
kilimfanya kuzomwa huku mchezaji huyo akitolewa mara moja kabla ya
Johann Berg Gudmundsson kuisawazishia Burnley ikiwa zimesalia dakika
nane.
Mkufunzi wa Burnley Sean Dyche alihisi kushindwa huko kwa Sterling kulibadilisha hali ya mechi hiyo.
Lakini Guradiola amesisitiza kuwa hakumtoa nje Sterling kwa sababu ya kukosa nafasi hiyo ya wazi.
Wakati huohuo Alexis Sanchez alifunga bao lake la kwanza akiichezea
Manchester United baada ya timu hiyo kuishinda Huddersfield na
hivyobasi kuisukuma katika eneo la kushushwa daraja.
Baada ya kipindi cha kwanza Romelu Lukaku aliipatia United uongozi kunako dakika 55 baada ya kupokea krosi nzuri.
Sanchez
baadaye alichezewa rafu na beki wa Huddersfield Michael Hefele na
hivyobasi kutunukiwa mkwaju wa penalti aliopiga ukapunguliwa na kipa
kabla ya kuupata na kufunga.


0 comments :
Post a Comment