
Ligi maalumu ya sikukuu ya krismas imeanzishwa wilayani ukerewe
mkoani Mwanza zikiwa ni jitihada za kuinua vipaji kwa vijana wilayani humo.
Michuano hiyo imeandaliwa na kituo cha kulea na kukuza vipaji cha
Victoria Youth Sport Academy(Viyosa)kwa udhamini wa Blog ya michezo inayoitwa
Boiplus.
Kivumbi cha michuano hiyo kinafanyika katika uwanja wa Getruda
Mongela mjini Nansio ikiwa imeanza 19/12 na tamati ni kwenye sikukuu za krismas
tar 25/12/2016 ambapo siku hiyo pia ni maalumu kwaajili ya kukitambulisha kituo
hicho cha michezo.
Katika mechi ya ufunguzi Viyosa fc imeibuka na ushindi kwa njia ya
penati 6-5 baada ya dakika 90 za sare ya bao 2-2 dhidi ya timu ya
Namagondo fc hivyo viyosa c imefuzu moja kwa moja kwenda nusu fainali.
Akizungumza na kipindi cha kona ya michezo cha 98.2 kwaneema fm
radio mkurugenzi wa kituo cha Viyosa Abdulaziz Makongo maarufu kama mwalimu
Dulah amesema kutokana na ligi hiyo kuchelewa kuanza wameona ni bora
wakaendesha mashindano hayo kwa mfumo wa mtoano.
Mwalimu dulah amesema michuano hiyo inashirikisha timu nane zote
za wilayani ukerewe kwa vijana wa umri chini ya miaka 17.
Timu zinazoshiriki katika michuano hiyo ni Viyosa fc,Namagondo
fc,Kagera fc,Yoso fc,Udc fc,Nantare fc,Butiliti fc na Boma fm.
Zawadi zitakazotolewa kwa msindi wa kwanza ni Tsh150,00/= Mshindi
wa pili ni Tsh100,000/= na Mshindi wa tatu ni Tsh50,000/=. Mfugaji bora
atachukua Tsh25,000/=
Hapa chini tumekuwekea picha za mechi hiyo ya ufunguzi,karibu
uzitazame:














0 comments :
Post a Comment