Mapema jana zilifanyika mechi mbili ambapo katika mechi ya kwanza Yosso fc iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera fc.Goli la kwanza lilifungwa na Seveline Costantine dk ya 75 huku la pili likifungwa naye Mazula Rinji dk 79.
Mechi ya pili ilizikutanisha timu za Boma fc vs Nantare fc ambapo Boma fc walitoka kidedea baada ya ushindi wa bao 2-0 wafungaji wakiwa ni Nyamasala Mgaya dk31 na Alex Palapala dk36 magoli yote yakitiwa kimiani kipindi cha kwanza.
Ligi hiyo inaingia mapumziko kwa siku ya leo na itarejea tena kesho tar 22/12/2016.
Ikumbukwe kuwa Timu zinazoshiriki katika michuano hiyo ni Viyosa fc,Namagondo fc,Kagera fc,Yoso fc,Udc fc,Nantare fc,Butiliti fc na Boma fm.
Zawadi zitakazotolewa kwa msindi wa kwanza ni Tsh150,00/= Mshindi wa pili ni Tsh100,000/= na Mshindi wa tatu ni Tsh50,000/=. Mfugaji bora atachukua Tsh25,000/=



0 comments :
Post a Comment