Viyosa fc imefanikiwa kuingia fainali baada ya kuifunga kwa penati 5-4 timu ya Yosso c katika mchezo wa nusu fainali uliofanyika katika uwanja wa getruda Mongela mapema jana.
Yosso fc ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli katika dk ya 7 kupitia kwa Seveline Constatine,Viyosa fc wakasawazisha kwa njia ya penati dk ya 13 mfungaji akiwa ni Abdallah Twaha ambapo Viyosa fc waliongeza goli la pili dk ya 32 likitiwa kimiani kitaalamu kabisa na Hamady Tungaraza maarufu kama Madizo.Yosso c wakasawazisha goli la pili kupitia kwa Emmanuel Humba maarufu kama chuji dk ya 60 hivyo kufanya matokeo kuwa 2-2 hadi mwisho wa mchezo.
Mikwaju ya penati ndiyo iliyoamua mshindi wa mchezo huo ambapo Viyosa fc ikatinga fainali baada ya kufunga penati 5-4.
Fainali ya michuano hiyo itakuwa ni tar 28/12 kwenye viwanja vya Getruda Mongela ambapo mshindi atapata kitita cha Tsh 150,000/= mshindi wa pili atapokea Tsh 100,000 mshindi wa tatu ataibuka na kitita cha Tsh 50,000/= huku Mfungaji bora akipata Tsh 25,000/=
Karibu sasa utazame picha mbalimbali katika mtanange huo wa nusu fainali.













0 comments :
Post a Comment