TAZAMA HII! KWANEEMA FM RADIO YAPATA MKURUGENZI MPYA


Bwn: PETER OMARY ambaye ni mkurugenzi mpya wa kwa neema fm akiwa katika pozi.




Marium Juma Mtaalamu wa masoko akiwa na mkurugenzi

Program menegerJackline Raphael akiwa na mkurugenzi
Mtaalamu wa kipindi cha full shangwe extra Joshua Dede akiwa na mkurugenzi
Chief Editor Jeston Kihwelo akiwa na mkurugenzi

Mtaalamu mwingine wa kipindi cha full shangwe extra Fabian Fanuel akiwa na mkurugenzi

Mtalamu wa kipindi cha michezo Erasto Juma akiwa na mkurugenzi
Mwanahabari Dominic Felician akiwa na mkurugenzi


Mtaalamu wa kipindi cha yaliyosheheni Specyoza Haule akiwa na mkurugenzi






Uongozi wa kituo cha redio kwaneema fm cha jijini mwanza umemtangaza  bwn:Peter Omary kuwa mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho ambaye atakuwa mtendaji mkuu katika uendeshaji wa redio hiyo.


Bwn: Peter Omary anachukua nafasi hiyo ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Askofu mkuu wa kanisa la TFE kwaneema bishop Augastine Mpemba ambaye yuko nje ya nchi kimasomo kwa muda mrefu sasa.


Akizungumza muda mfupi baada ya kutangazwa rasmi mbele ya wafanyakazi wa kituo hicho Bwn: Omary amesema atahakikisha kituo hicho kinawanufaisha watanzania walio wengi kutokana na mikakati mipya mbalimbali ilofikiwa ikiwa ni pamoja na kupitia upya vipindi vya redio kwa lengo la kuviboresha zaidi.


Aidha Bwn: Omary amewataka wasikilizaji wa 98.2 kwaneema fm radio kuendelea kukiunga mkono kituo hicho likiwemo tamasha la miaka 5 tangu kuanzishwa kwake litakalofanyika JB Belmont hotel 6/4/2015 kwa kuendelea kununua tiketi kwa wingi, ambapo pia amesema hakuna kitakachobadilika bali ubora wa kituo kuongezeka kwa kasi siku hadi siku.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment