NA: JACKTAN MSAFIRI
Mashindano ya rock city marathon yamefanyika hapo jana katika barabara nbalimbali za jiji la Mwanza yakihitimishwa katika viwanja vya ccm kirumba huku yakihudhuliwa na watazamaji mbalimbali waliojitokeza kutazama.
Katika mashindano hayo jiji la Mwanza halikufanya vizuri katika ushindi wajuu ambapo mshindi wa kwanza katika km 21 kwa upande wa wanamme ni
Joseph Panga alikitokea manyara,nafasi ya pili ilichukuliwa na Sammy Nyakoye kutoka Kenya na wa tatu akiwa ni Festus Talam kutoka Kenya.
Joseph Panga alikitokea manyara,nafasi ya pili ilichukuliwa na Sammy Nyakoye kutoka Kenya na wa tatu akiwa ni Festus Talam kutoka Kenya.
Upande wa wanawake km 21 mwanamama Marhalia Elisante kutoka Manyara alikamata nafasi ya kwanza,nafasi ya pili ilikwenda kwa Mary Naali kutoka Arusha huku watatu akiwa Adelina Audata kutoka Kilimanjara
-Mtanzania Joseph Panga kutoka Manyara Tanzania mshindi wa mbio za Rock City Marathon akizungumza na vyombo vya habari
-Mshindi wa kwanza mbio za Kilometa 21 wanawake ni Mathalia Elisante kutoka
Manyara Tanzania aliyetumia muda wa saa 1:14:25
-Mshindi wa kwanza Kilomita 2 watoto upande wa wasichana ni Irene Fidelin.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na Jesca Amos huku nafasi ya tatu ikikamatwa na Janeth Charles.
-Rais wa Shirikisho la Riadha nchini Tanzania Andrew Mtaka (nyuma) akiongoza picha ya pamoja na watoto washindi upande wa wavulana mbio za Kilomita 2 ambapo Masumbuko Julias aliibuka mshindi,nafasi ya pili ikishikwa na Medadi Paulo, ya tatu ni Festo Daniel.
-Rais wa Shirikisho la Riadha nchini Tanzania Andrew Mtaka (kulia nyuma)akiongoza picha ya pamoja na washindi wa Rock City Marathon Kilomita 5 wanawake Albino ambapo mshindi wa kwanza alikuwa Irene Joseph, wa pili ni Asteria Abel huku nafasi ya tatu ikishikwa na Saidati Haji.
-Rais wa Shirikisho la Riadha nchini Tanzania Andrew Mtaka akifuatiwa na Meneja Kiongozi NSSF Mwanza Hamis Faki katika picha ya pamoja na washindi nafasi za juu Rock City Marathon Kilomita 5 wanaume Albino ambapo Paschal Charles kutoka Magu Mwanza aliibuka mshindi, nafasi ya
pili ikikamatwa na Paschal Emmanuel naye kutoka Magu na ya tatu ikichukuliwa na George Joseph wa Ilemela Mwanza.
-Picha ya washindi na meza kuu ambapo mshindi wa kwanza mbio za Kilometa 21wanawake ni Mathalia Elisante kutoka Manyara Tanzania (kulia mwenye track suit ya njano) aliyetumia muda wa saa 1:14:25.Wa pili niMary Naali Tz (katikati) aliyetumia muda wa saa 1:15:34 Wa tatu ni Adelina Audata Tz (kushoto) aliyetumia muda wa saa 1:23:01
-Mtanzania Joseph Panga kutoka Manyara Tanzania mshindi wa mbio za Rock City Marathon akikimbia Kilomita 21 Wanaume kwa kutumia muda wa saa 1:02:36 akionyesha kitita chake shilingi za Kitanzania milioni 1.5 Nafasi ya pili ilichukuliwa na Sammy Nyakoye kutoka Kenya 1:02:39 zawadi ya shilingi za Kitanzania laki 9 Ya tatu ni Festus Talam kutoka Kenya 1:15:34. aliyepata zawadi ya shilingi laki 7 za Kitanzania.
-Rais wa Shirikisho la Riadha nchini Tanzania Andrew Mtaka akizungumza na wadau waliohudhuria Rock City Marathon 2014 uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
-Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Amina Masenza akihutubia umma uliojitokeza kushuhudia Rock City Marathon 2014 katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, ambapo moja kati ya ahadi aliyoweka amesema kuwa Ofisi yake itajipanga mwakani kuona ni jinsi gani inaweza kuboresha zaidi
mashindano hayo ili yapate msisimko zaidi na hata kushuhudia baadhi ya wadau toka ofisi yake wakishiriki, kwani yanatumika kuitangaza wilaya yake.
PICHA: KWA HISANI YA GSENGO BLOG
















0 comments :
Post a Comment