MBIO ZA ROCK CITY MARATHON KUFANYIKA OCT 26 2014 CCM KIRUMBA!
Mashindano ya riadha ya rock city marathon yanatarajia kufanyika 26/10/2014 katika viwanja vya ccm kirumba yakiwa nanafanyika kwa mara ya sita sasa.
Akizungumza na wandishi wa habari za michezo wa mkoa wa mwanza mapema jana mratibu
wa mbio hizo kutoka kampuni ya CAPITAL PLUS INTERNATION bwn: Methew Kasonta amesema mwaka huu katika mbio hizo kutakuwa na mashindano katika mbio za km 12, km5 kwaajili ya makampuni na walemavu wa ngozi(albino)
km3 kwaajili ya wazee km2 kwaajili ya watoto pamoja na mbio fupi za uanjani mita 100, m400 na m1500
Aidha kasonta alisema mshindi wa kwanza katika mbio za km12 atapata zawadi ya
sh. ml 1 na laki 5 mshindi wa pili laki tisa wa tatu laki 7 wa nne na wa tano laki 1 huku wa sita hadi kumi wakipata elfu hamsini.
katika mbio za km5 msindi wa kwanza atapata Tsh 50,000/= wa pili 30,000/= na wa
tatu 20,000/=
Kasonta aliendelea kwa kusema msindi wa kwanza katika mbio za km 3 maalum kwa wazee na km3 kwa watoto atapata Tsh. 50,000/= Wa pili 30,000/= wa tatu 20,000/= huku weanne hadi wa kumi 10,000/=.na katika mbio fupi za uanjani mita 100 mshindi wa kwanza atapata Tsh40,000/= wa pili 25,000/= wa tatu 15,000/= kwenye mita 400 wa kwanza atapata 40,000/= wa pili 25,000/= wa tatu 15,000/= na katika mita 1500 wa kwanza atapata 40,000/= wapili
25,000/= na wa tatu 15,000/=
-kutoka kushoto ni methew kasonta akifatiwa na gibson mtaegea wakati wakizungumza na wanahabari
Akiyataja maeneo yatakayopitiwa katika mbio hizo mjumbe wa kamati ya rock city marathon mkoa wa mwanza bwn:Gibson Mtaegea alisema mbio za km 21 zitaanzia uanja wa ccm kirumba hadi round about ya samaki,mbio za km5
zitaanzia mabatini hadi ccm kirumba mbio za km3 zitaanzia makaburi ya wahindi(mt.meru filling station) hadi ccm kirumba wakati mbio za watoto za km2 zitaanzia mwaroni hadi ccm kirumba.
Bwn:Gibson alisema fomu za ushiriki kaika mbio hizo zinapatikana katika uanja wa nyamagana jijini mwanza huku akiainisha gharama kuwa katika km12 gharama ya fomu ni Tsh 5,000/= km3 3,000/= na km 2 ni 2,000/=
Kwaupande wake katibu mkuu wa chama cha riadha Tanzania Suleyman Nyambui amewataka wakazi wa jiji la mwanzakushiriki kwa wingi katika mchezo huo kwa kuchukua fomu ama kujitokeza kwa wingi siku ya tukio kwaajili ya kuwashangilia washiriki na kuwatia moyo kwani kwa kufanya hivyo pekee kutatia hamasa na kuendeleza mchezo wa riadha na kuufanya upige hatua kama ilivyo katika mkoa wa kilimanjaro ambao umeendelea sana katika riadha.
-suleyman nyambui akizungumza na wanahabari







0 comments :
Post a Comment