LIGI KUU VODACOM VPL:VIWANJA 4 LEO KUWAKA MOTO,AZAM FC KUJIULIZA KWA WAPIGA KWATA WA JKT MGAMBO KUTOKA TANGA.












LEO Viwanja vinne vitashuhudia Mechi 4 za Ligi Kuu Vodacom ambazo ni Mechi za Nane kwa kila Timu lakini Wakongwe na Vinara wa Ligi, Simba, na Yanga, ambao ni Mabingwa Watetezi na pia wapo Nafasi ya Pili, hawapo dimbani hadi Wikiendi hii.

Katika Mechi za leo, JKT Ruvu, ambao wako Nafasi ya Tatu, wapo Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu.
Huko Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Mjini Tabora, Timu zilizopanda Daraja Msimu huu, Rhino Rangers na Mbeya City, zitacheza.

Nao JKT Oljoro, ambao wako kwenye Nafasi ya 12, watakuwa Wenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Azam FC, ambao wako Nafasi ya Nne, wapo kwao Azam Complex, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, kucheza na Mgambo JKT ambayo iko Nafasi ya 13 ikiwa Nafasi moja tu toka Mkiani.

Ligi hi itaendelea tena Jumamosi kwa Mechi mbili za Wakongwe Yanga na Simba kucheza Mechi zao huko Bukoba ambako Yanga wataivaa Kager Sugar na Jijini Dar es Salaam, Simba watacheza na Tanzania Prisons.

RATIBA:
Jumatano Oktoba 9
Rhino Rangers v Mbeya City
JKT Oljoro v Ruvu Shooting
Azam FC v Mgambo JKT
Mtibwa Sugara v JKT Ruvu

RATIBA:
Jumamosi Oktoba 12
Kagera Sugar v Yanga
Simba v Tanzania Prisons
Jumapili Oktoba 13
Ashanti United v Coastal Union
Ruvu Shooting v Rhino Rangers
Mgambo JKT v Mbeya City
Azam FC v JKT Ruvu
Mtibwa Sugar v JKT Oljoro
VPL-MSIMAMO:
NA TIMU P W D L GD GF POINTI
1 Simba SC 7 4 3 0 11 16 15
2 Yanga SC 7 3 3 1 6 13 12
3 JKT Ruvu 7 4 0 3 4 8 12
4 Azam FC 7 2 5 0 3 9 11
5 Coastal Union 7 2 5 0 3 6 11
6 Mbeya City 7 2 5 0 2 8 11
7 Kagera Sugar 7 3 2 2 2 7 11
8 Ruvu Shooting 7 3 1 3 2 7 10
9 Rhino Rangers 7 1 4 2 -1 7 7
10 Mtibwa Sugar 7 1 4 2 -3 5 7
11 Prisons FC 7 1 4 2 -5 4 7
12 JKT Oljoro 7 1 2 4 -3 4 5
13 Mgambo JKT 7 1 2 4 -9 2 5
14 Ashanti United 7 0 2 5 -11 4 2
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment