VPL: MABINGWA WATETEZI YANGA WASHUSHWA CHINI,AZAMU,MBEYA CITY NI MOTO WA KUOTEA MBALI SASA ZAIPUMULIA JUU JUU MNYAMA SIMBA!!!!!







<<<<<MTIBWA YATANDIKA BAO 5 HUKO MANUNGU!

VPL, Ligi Kuu Vodacom, imeendelea jana kwa Mechi 4 na ushindi kwa Azam FC na Mbeya City zimeifanya Timu hizo ziivute chini Yanga kutoka Nafasi ya Pili ingawa Yanga imecheza Mechi moja pungufu huku Simba wakiendelea kubaki kileleni.

Azam FC, wakicheza kwao Azam Complex, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, waliichapa JKT Ruvu Bao 3-0 kwa Bao za John Bocco, Dakika ya 12, Erasto Nyoni Dakika ya 39 na Salum Abubakar  Dakika ya 90.

Huko Mabatini,  Mlandizi, Mkoani Pwani, Elias Maguri aliipa ushindi Ruvu Shooting kwa kufunga Bao pekee la Mechi hiyo katika Dakika ya 77 walipocheza na Rhino Rangers ya Tabora.
Nayo Mbeya City, ikicheza huko Mkwakwani Tanga, iliitungua Mgambo JKT Bao 1-0 kwa Bao la Jeremiah John.

Huko Manungu, Morogoro, Mtibwa Sugar iliitandika JKT Oljoro Bao 5-2 huku Mchezaji wao Abdallah Juma akipiga Hetitriki na Bao nyingine kutumbukizwa na Juma Luizio wakati Bao za JKT Oljoro kuingizwa na Shaibu Nayopa na Amir Omar.

MATOKEO:
Jumapili Oktoba 13
Ruvu Shooting 1 Rhino Rangers 0
Mgambo JKT 0 Mbeya City 1
Azam FC 3 JKT Ruvu 0
Mtibwa Sugar 5 JKT Oljoro 2

RATIBA:
Jumatano Oktoba 16
Ashanti United v Tanzania Prisons
Jumamosi Oktoba 19
Kagera Sugar v Coastal Union
JKT Oljoro v Azam FC
Mtibwa Sugar v Mgambo JKT
Mbeya City v JKT Ruvu
Ashanti United v Ruvu Shooting
Jumapili Oktoba 20
Simba v Yanga
VPL-MSIMAMO:
NA TIMU P W D L GD GF POINTI
1 Simba SC 8 5 3 0 12 17 18
2 Azam FC 9 4 5 0 8 14 17
3 Mbeya City 9 4 5 0 5 12 17
4 Yanga SC 8 4 3 1 7 15 15
5 Ruvu Shooting 9 4 2 3 3 10 14
6 Mtibwa Sugar 9 3 4 2 1 10 13
7 JKT Ruvu 9 4 0 5 0 9 12
8 Coastal Union 8 2 5 1 2 7 11
9 Kagera Sugar 8 3 2 3 1 8 11
10 Rhino Rangers 9 1 4 4 -4 8 7
11 Prisons FC 8 1 4 3 -4 4 7
12 JKT Oljoro 9 1 3 5 -6 8 6
13 Ashanti United 8 1 2 5 -10 6 5
14 Mgambo JKT 9 1 2 6 -16 2 5
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment