Mchezo huo wa ligi kuu bara unatarajiwa kuchezwa saa 8 mchana siku ya
Jumapili, awali mchezo huo ulikuwa uchezwe siku ya Jumamosi lakini
ratiba ilibadilishwa kutokana na maombi ya Mtibwa Sugar kuomba mchezo
huo upelekwe siku ya Jumapili.
Sababu ya wana tam tam kuomba mabadiliko hayo ya ratiba ni kutokana
na safari ndefu ya kutoka Lindi walipokuwa wameenda kucheza mchezo wa
kombe la shirikisho dhidi ya Maji Maji Rangers ambao wana tam tam wali
ibuka na ushindi wa goli 1-2, safari hiyo inawalazimu wana tam tam
kufika mkoani Shinyanga siku ya Ijumaa na siku ya Jumamosi ambayo
ilikuwa siku ya mchezo wenyewe wanaitumia kwa mapumziko na hivyo mchezo
huo wa raundi ya 16 unatarajiwa kuchezwa Jumapili saa 8:00 mchana.
Mabingwa wa ligi kuu bara wanaoneka kuwa bora na kuimalika zaidi
msimu huu baada ya kufanikiwa kukusanya pointi 26 katika michezo 15 ya
ligi kuu bara huku wapinzani wao wakifanikiwa kukusanya pointi 13 katika
michezo 15 ya ligi kuu bara.
Kikosi cha wana tam tam kipo kamili na wachezaji wote woko katika
hali nzuri ya kuendelea kupambana isipokuwa Riphat Khamis aliyeumia
katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City.

0 comments :
Post a Comment