MKUTANO WA CHADEMA MWANZA:M4C YAENDELEA,MATOKEO YA KUSIKITISHA YA KIDATO CHA 4 YAWALIZA WANANCHI,WAZIRI SHUKURU KAWAMBWA ATAKIWA KUJIUZULU.


MWENYEKITI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA BW FREEMAN MBOWE AMEWATAKA VIONGOZI WA CHAMA HICHO NGAZI MBALIMBALI KUWA MFANO WA KUIGWA KATIKA KUTETEA NA KULINDA MASLAHI YA WANANCHI ILI KUCHOCHEA MAENDELEO YA TAIFA

BW MBOWE AMETOA KAULI HIYO JANA TAREHE 20 FEBRUARI,2013 ALIPOZUNGUMZA NA VIONGOZI WA CHADEMA WA MIKOA YA KANDA YA ZIWA MAGHARIBI JIJINI MWANZA WAKATI WA UZINDUZI WA VUGUVUGU LA MABADILIKO (M4C) KATIKA KANDA HIYO INAYOJUMUISHA MIKOA YA MWANZA, KAGERA NA GEITA

AMEWATAKA VIONGOZI WA CHAMA HICHO KUZINGATIA UTAWALA BORA KATIKA SHUGHULI ZAO HUKU AKIWASIHI KUEPUKA MAMBO YANAYOWEZA KUKIGAWA CHAMA HICHO HALI INAYOWEZA KUTUMIWA NA VYAMA PINZANI KUKINYONG’ONYEZA CHADEMA
 
HATA HIVYO JIONI CHAMA CHA DEMOKRASIA  NA MAENDELEO KILIPATA FURSA YA KUZUNGUMZA NA WANANCHI KATIKA VIWANJA VYA FURAHISHA AMBAPO  BWANA FREEMAN MBOWE AMEWATAKA
WANANCHI  KUWA IMARA NA KUTOYUMBISHWA NA WANASIASA WACHOCHEZI  NA  KUEPUKA KUSHIRIKI KATIKA MIGOGORO YA KIDINI ILIYOENDELEA NCHINI..

 BWANA MBOWE  HAKULIACHA NYUMA SUALA LA MATOKEO YA KIDATO CHA  NNE   AMBAPO AMEMTAKA  WAZIRI WA ELIMU SHUKURU KAWAMBWA KUJIHUDHULU.
Hawa ni wananchi wa Jijini Mwanza wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Bw. Freeman Mbowe katika mkutano wa Hadhara kwenye viwanja vya FURAHISHA Jijini Mwanza.
Wafuasi wa Chama cha Democrasia na Maendeleo(CHADEMA) wakichangia kapu la M4C katika Mkutano wa CHADEMA uliofanyika jana Februari 19,2013 kwenye viwanja vya FURAHISHA Jijini Mwanza.
 Mwenyekiti wa CHADEMA TAIFA Freeman Mbowe wa pili kutoka (kulia) akipeana tano na wafuasi wa chama hicho katika viwanja vya furahisha, wa kwanza kutoka (kulia) ni Mbunge wa jimbo la Nyamagana Hezekia Dibogo Wenje,na wa kwanza kushoto ni Mbunge wa jimbo Ilemela Highness Kiwia wote wa CHADEMA.
                                        Inaashiria wakiteta jambo eeeeeeh?
Huu ndo umati wa mahudhurio ya wafuasi wa CHADEMA katika viwanja vya FURAHISHA Jijini Mwanza katika Mkutano wa chama hicho.
                      Nipe tano kiongozi !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!














Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment