AFCON 2015 NCHINI MOROCCO: CAF YAPANGA VYUNGU VYA DROO, TANZANIA HAIMO, KUANZA AWALI!

<<<<<<<<VYUNGU VITATU VYA TIMU 11 KILA KIMOJA VYATAJWA!!
<<<<<<<<BONGO WAPO CHA 4 WAKIPITA RAUNDI YA AWALI!
AFCON_2015_LOGO-MOROCCOSHIRIKISHO la Soka Afrika, CAF, leo limetangaza mgao wa Vyungu kwa ajili ya kufanya Droo kwa ajili ya Mechi za Makundi ili kupata Timu 15 zitakazojumuika na Wenyeji Morocco kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015 na Tanzania haimo kwenye Timu 33 zilizopangwa Vyungu Vitatu ikimaanisha itabidi waanze  hatua ya awali kabisa ili kufuzu kuingizwa kwenye Droo.
Droo ya kupanga Makundi na Mechi za Raundi ya Awali itafanyika hapo Machi 10.
Mabingwa wapya wa Afrika, Nigeria, pamoja na waliovuliwa Taji, Zambia, na Vigogo wengine wapo Chungu Namba 1 ikimaanisha Timu hizi haziwezi kuwekwa Kundi moja.

VYUNGU:
CHUNGU 1: Nigeria, Burkina Faso, Cote d’Ivoire, Togo, Mali, South Africa, Cape Verde, DR Congo, Zambia, Tunisia, Ghana.
CHUNGU 2: Egypt, Libya, Algeria, Senegal, Cameroon, Guinea, Sierra Leone, Gabon, Uganda, Congo, Central African Republic.
CHUNGU 3: Ethiopia, Benin, Angola, Niger, Zimbabwe, Equatorial, Mozambique, Malawi, Burundi, Liberia, Sudan.
CHUNGU 4: Timu 11 zitakazofuzu Raundi ya Awali
FAHAMU:
-Kundi litakuwa na Timu 4 na Makundi yatapangwa kwa kuchukua Timu moja toka kila Chungu.
-Hivyo, Timu za Chungu kimoja haziwezi kuwa Kundi moja.

Nchi ambazo zinatarajiwa kucheza Raundi ya Awali kwa Mtindo wa Mtoano wa Nyumbani na Ugenini ni 21 na nazo ni Tanzania, Botwsana, Chad, Kenya, Sao Tome & Principe, South Sudan, Comoros, Lesotho, Madagascar, Mauritania, Somalia, CAR, Djibouti, Eritrea, Gambia, Guinea Bissau, Mauritius, Namibia, Rwanda, Seychelles, Swaziland.
Hii inamaanisha Mpinzania wa Tanzania katika Raundi ya Awali anaweza kuwa yeyote kati ya Timu 20.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment