MKAZI WA
KIJIJI CHA NYANKORONGO WILAYANI CHATO LAMECK MARABA (29) AMEJIUA KWA KUJIKATA
KOROMEO BAADA YA KUHISI ANA UGONJWA WA UKIMWI MUDA MFUPI BAADA YA KUSHAURIWA NA
DAKTARI KUPIMA AFYA YAKE.TUKIO HILO
LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA JANA BAADA YA KIJANA HUYO KUSHITUSHWA NA USHAURI WA
DAKTARI ALIYEMTAKA KUPIMA AFYA YAKE ILI KUBAINI MAGONJWA YANAYOMKABILI
MGANGA
MFAWIDHI WA HOSPITALI YA WILAYANI YA CHATO BWANA PIUS BUCHUKUNDI AMESEMA
MGONJWA HUYO ALIFIKA HOSPITALINI HAPO JANUARI 17 AKISUMBULIWA NA HOMA YA
MATUMBO, MALARIA NA UPUNGUFU WA DAMU AMBAPO KUTOKANA NA HALI HIYO ALISHAURIWA
KUPIMA VVU
AMEONGEZA
KUWA KUTOKANA NA USHAURI HUO ALIINGIWA HOFU NA NDIPO KUAMUA KUJIKATA KOROMEO NA
KUSABABISHA KIFO CHAKE.
PAMOJA NA
HILO MGANGA HUYO AMETOA USHAURI KWA WAGONJWA WANAOKWENDA KUTIBIWA WAFUATE
USHAURI UNAOTOLEWA NA WAUGUZI ILI KUEPUSHA VIFO VISIVYO VYA LAZIMA.
JESHI LA
POLISI WILAYANI CHATO LIMETHIBITISHA KUTOKEA KWA KIFO HICHO CHA KUSIKITISHA.
0 comments :
Post a Comment