Spika
wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili leo Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kupokelewa na Kaimu Balozi wa Tanzania
nchini humo Bwana Hemed Mgaza (katikati) Kushoto ni Mwenyekiti wa Bunge
na Makanu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulizi na
Usalama Mhe. Musa Azzan Zungu (Mb). Kulia ni Mhe. Sadifa Juma Khamis,
(Mb).Mhe. Spika ameongoza ujumbe wa Wabunge watano kudhuria Mkutano wa
tatu wa Kimataifa wa Jukwaa la Kibunge la nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Jukwaa
la Mabunge ya Jumuiya ya Kimataifa ya nchi za Ukanda wa Maziwa Mkuu
(FP-ICGLR) limeitaja Tanzania kuwa mfano wa kuigwa kwa juhudi
inazozifanya kuleta amani barani Afrika. Pongeli hizi zimetolewa leo na
jumla ya nchi wa kumi na mbili zinazounda Jukwaa hilo kwenye mkutano wa
tatu unaoendelea kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
zimewataja Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete
pamoa na watanzania kama wapenda amani barania Afrika. Hii ni kutokana
na viongozi hao kujitolea kusuluhisha migogoro ya DRC/Rwanda na kundi la
M23, migogoro ya Afrika ya Kati, mgogoro wa Sudani na Sudani Kusini,
mgogoro wa Kenya baada ya uchaguzi mkuu na mingine mingi. Pamoja na
Tanzania, Afrika Kusini nayo imepongezwa. Bunge la Tanzania limewkilishwa
na Spika wa Bunge Anne Makinda ambaye ameongoza ujumbe wa wabunge watano ambao ni
Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mhe. Pauline Gekul, na Mhe Sadifa Juma. Wengine
ni Mhe. Mohamed Mbarouk na Mhe. Prudenciana Kikwembe.
Spika Makinda na Spika wa Kenya Mhe. Kenneth Marende (kulia) wakiingia kwanye mkutano huo.
Ufunguzi wa mkutano wa Tatu wa PF –ICGLR (Forum of Parliaments of International Conference on Great Lakes Region – FP/ICGLR) mjini Kinshasa
Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo
Picha ya pamoja ya maspika, Sekretarieti pamoja na washirika wa maendeleo wa FP-ICGLR
(Picha na Prosper Minja-Bunge) kwa hisani ya FULL SHANGWE BLOG.
0 comments :
Post a Comment