Kipa wa Sudan Akram El Hadi aliokowa
mikwaju miwili ya penalti wakati timu yake ilipoishinida Libya na
kuibuka nafasi yatatu katika mashindano ya ubingwa wa mataifa ya Afrika
(CHAN).
Mechi ilimalizika kwa sare ya 1-1 baada ya dakika 90 huko Marrakech.
Awali
Akram alishindwa kuihimili krosi kutokakwa Salem Ablo iliochangia sare
hiyo kwa Libya zikiwa zimesalia dakika sita tu kwa mechi kuisha.
Sudan iliongozwa kunako dakika nane wakati Walaa Eldin Musa alipotikiza wavu kutokana na hedi aliyoipiga.
Katika awamuya mikwaju ya penalti , Sudan ilifanikiwa kusukuma
mikwaju yote minne ndani huku mikwaju ya Elmehdi Elhouni na Ablo
ikizuiwa na Akram.
Ni shaba ya pili kwa Sudan katika fainali za
mshindani hayo ya CHAN baada ya kuibuka tena nafasi ya tatu walipokuwa
waandalizi wa mashndano hayo mnamo 2011, huku Libya wakiibuka mabingwa
miaka mitatu baada ya hapo.

0 comments :
Post a Comment