Beki wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Godin hapo jana siku ya Jumapili
alijikuta akitokwa na meno baada ya kumng’ata golikipa wa Valencia
katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania Laliga.
Klabu hiyo ya Atletico imetoa taarifa kuwa Godin amefikishwa katika
hospitali ya meno jijini Madrid kufuatia dhahama hiyo huku timu hiyo
ikiibuka na ushindi wa bao 1 – 0 katika dimba la Wanda Metropolitano.
Baada ya tukio hilo ililazimika Godin afanyiwe mabadiliko haraka mapema
mwa kipindi cha pili cha mchezo huo huku wakati tukio hilo likiwa
limetokea wakati mlinda lango wa Valencia Neto akiokoa mpira wa hadhabu.



0 comments :
Post a Comment