SINGIDA UNITED IMEIKAMATA AZAM FC BAADA YA USHINDI WAKE DHIDI YA MBAO FC.

Klabu ya soka ya Singida United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Mbao FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba ikiwa ni mwendelezo wa mechi za ligi kuu soka Tanzania Bara.


Katika mchezo huo wa raundi ya 17, Singida United walifanikiwa kufunga bao la kwanza dakika ya 45 kupitia kwa Shafik Batambuze kabla ya Mbao FC kusawazisha kupitia kwa Habib Kiyombo dakika ya 51.

Singida United walijihakikishia ushindi dakika ya 58 kupitia bao la Deus Kaseke ambalo limewapa alama tatu muhimu na kuwafikia Azam FC kwa alama 33.

Azam FC wamepoteza mechi yao ya raundi ya 17 dhidi ya Simba hivyo kubaki na alama 33 katika nafasi ya tatu wakilingana na Singida United.


Share on Google Plus

About Tiktak

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment