Habari kutoka Hispania zinaeleza kuwa meneja wa zamani wa klabu ya
Barcelona, Luis Enrique ameonekana kukubali kurithi mikoba ya kocha
Antonio Conte ndani ya Chelsea.
Nafasi ya Conte ndani ya kikosi cha Blues imeonekana kuwa mashakani
tangu wiki iliyopita baada ya kupata matokeo mabaya ya kufungwa 3 – 0
dhidi ya Bournemouth na yale ya 4-1 mbele ya Watford siku ya Jumatatu.
Kufuatia mwenendo wa kusuasua kwa kikosi cha Chelsea mmiliki wa timu
hiyo Mromania Abramovich anampango wa kumpatia mkataba wa miaka miwili
na nusu kocha Enrique mwenye umri wa miaka 47 ambao atakuwa the blues
hadi mwaka 2020 hii ni kwa mujibu wa chombo cha Sports.



0 comments :
Post a Comment