Akizungumza na Tiktaktz Maguli
amesema, Mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Cosafa mwezi Juni Mwaka jana
nchini Africa kusini, alisaini nao mkataba wa awali Mara baada
ya kiridhishwa na kiwango chake lakini maslahi waliyokubaliana yalikiwa tofauti
katika mkataba wa pili.
"Nilishasaini nao mkataba wa
awali na tulikubaliana nilirudi kumalizana nao lakini katika awamu ya pili
ilikuwa tofauti na ikumbukwe kipindi kile kilikuwa ni cha siasa Africa kusini
na mwenyekiti wa Palokwane ni kiongozi wa siasa na ndiye mtoaji wa pesa kwahiyo
nilipofika kulikuwa na mabadiliko kuhusu kiwango cha pesa tulichokubaliana
ambapo kulikukuwa na mapungufu, "
Maguli amesema walijaribu kukaa na
kuongea ikiwa ni pamoja na kupiga hesabu ya pesa inayobakia na kuona
bado haitoshi ukitoa kodi ambayo kwa mchezaji binafsi ni kubwa kwani mchezaji
anatakiwa kujilipia kodi pamoja na kukodi gari suala ambalo
walishindwana.
Maguli amesema, aliamua kuondoka na
kurudi Tanzania ambapo alikuta dirisha dogo la usajili limesogezwa mbele, na
wakati bado yupo Tanzania Meneja wake alipigiwa simu kumtaka kurejea Afrika
kusini ili asaini mkataba wa muda mfupi huku wakiangalia hali itakuwaje
baada ya kumaliza mkataba huo ambapo uongozi wa Polokwane ulikataa na kumtaka
asaini miaka mitatu kitu ambacho kilishindikana.
Kwa sasa Maguli bado
yupo Tanzania na Meneja wake anaenndelea na taratibu za kumtafutia timu
nyingine katika dirisha la usajili msimu ujao huku Maguli mwenyewe akisema yupo
tayari kuichezea timu yoyote ya ndani au nje ya mipaka ya Tanzania iwapo
wataafikiana kimaslahi.

0 comments :
Post a Comment