Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amepongeza uongozi wa timu hiyo
kufuatia kuachana na mazungumzo ya kunasa saini ya Riyad Mahrez wa
klabu ya Leicester.
City iliachana na dili hilo kufuatia Leicester kuhitaji kiasi cha paundi milioni 95 swala ambalo liligonga mwamba.
Uongozi wa Man City, uliandaa kiasi cha paundi milioni 65 ili
kumsajili staa huyo wa Algeria kitita ambacho kilikataliwa na
Leicester City na hivyo kujitoa katika kinyang’anyiro cha mchezaji huyo
hapo jana siku ya Jumatano wakati wa kufungwa kwa dirisha la usajili.
“Nimevutiwa na maamuzi yaliyofikiwa na klabu yangu kuachana na dili
hilo, pengine katika kipindi kijacho tuta nunua mchezaji kwa gharama
hiyo ya paundi milioni 100 lakini sio kwa wakati huu,”amesema Guardiola.


0 comments :
Post a Comment