MJUMBE wa kamati ya utendaji ya Simba, Musleh Al Rawah amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijin Dar
es salaam leo kwa shtaka la kumjeruhi mtoto wa mwenyekiti wa Yanga,Yusuph Manji.
Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Genis Tesha alidai kuwa Al Rawah alifanya kosa hilo, Machi 8, 2015 kwenye Uwanja wa Taifa uliopo Chang'ombe.
Tesha alidai kuwa siku hiyo ya tukio, mshtakiwa Al Rawah alimpiga teke Meheub Manji na katika sehemu nyingine mbalimbali za mwili ukiwamo uso na kumsababishia
majeraha mazito.
Al Rawah ambaye ni mfanyabiashara na mmoja wa viongozi ndani ya klabu ya Simba anayetetewa
na Wakili Damas Ndumbalo, alilikana shtaka hilo na upande wa mashtaka ukadai kuwa upelelezi wa kesi hiyo badohaujakamilika,hata hivyo baada ya mshtakiwa kusomewa shtaka hilo,upande wa mashtaka uliiambia mahakama
kuwa hauna pingamizi na dhamana.
Kwa upande wa Wakili Ndumbalo naye aliomba mteja wake apewe dhamana.
Hakimu Frank Moshi akitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa huyo, alimtaka awe na mdhamini mmoja ambaye anatoka katika taasisi inayotambulika na serikalini.
Baada ya mdhamini kujitokeza upande wa mashtaka ulizifanyia uhakiki barua hizo ndani ya saa moja kama ilivyoelekezwa na mahakama na mshtakiwa akaachiwa huru.
Kesi imeahirishwa hadi Aprili 20,2015 kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi umekamilika ama la.
KWA HISANI YA:michuzi blog
0 comments :
Post a Comment