NI BONGE LA MECHI KATIKA UKANDA WA ZIWA TWIGA STARS V/S WANAHABARI WA MWANZA!



NA:   JACKTAN MSAFIRI,Mwanza


KUTOKANA NA KANDA YA ZIWA KUWA NA IDADI KUBWA YA AKINA MAMA WAGONJWA WA KANSA YA SHINGO YA KIZAZI kampuni ya BORN TO HELP-TANZANIA ikishirikiana na KONA YA MICHEZO ya kwaneema fm radio wameandaa mechi kubwa ya kijamii jijini Mwanza na Kanda ya Ziwa,ambapo Timu ya
Taifa ya Wanawake "TWIGA STARS" watapambana na mashujaa wa kalamu na sauti(VOCALISTS)WAANDISHI WA HABARI NA
WATANGAZAJI MKOA WA MWANZA jumapili 5/10/2014 katika dimba la CCM Kirumba Mmwanza saa 10:00 jioni.


Akizungumza na wanahabari mkurugenzi wa BORN TO WIN FOUNDATION ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha kona ya michezo katika kituo cha kwa neema fm radio ERASTO JUMA amesema kutakuwa pia na Mechi ya utangulizi kati ya Wanakesha mapanda TOTOAFRICANS V/S Matajiri wa ALLMAS MWADUI FC saa 8:00 Mchana.
   -Mkurugenzi wa  BORN TO HELP FOUNDATION Erasto juma akizungumza na wanahabari.

Aidha ERASTO amesema asilimia kubwa ya mapato itamsaidia mama mgonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi ambapo kauli mbiu ya mchezo huo wa kijamii ni  "tuunganena kupiga vita kansa ya shingo ya kizazi'.NANI KAMA MAMA!    

Kwa upande mwingine erasto amesema viingilio katika mechi hiyo vitatajwa hivi karibuni,huku akiwataka wadau, taasisi na kampuni binafsi kujitokeza kudhamini mchezo huo kwa kuwasiliana naye kwa namba ya simu 0767 200 986
                            
Naye mratibu wa timu ya wanahabari jijini mwanza BWN: EDWIN SOKO amewataka wakazi wote wa jiji la mwanza kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ambao ni maalum kwa jamii,huku akisema timu ya wanahabari iko tayari kabisa kuelekea mchezo huo.
                           -Edwin soko akizungumza na wanahabari
    -wandishi wa habari wakifuatilia kwa makini taarifa ya ujio wa twiga stars
                                        
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment