GUS POYET ANUKIA SUNDERLAND.

NAHODHA MANCHESTER CITY VINCENT KOMPANY NJE WIKI 4

Sunderland wapo mbioni kumtangaza Meneja wa zamani wa Brighton, Gus Poyet, kama Meneja wao mpya.
Sunderland, ambao wako mkiani kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na Pointi 1 katika Mechi 7, walimtimua Paolo Di Canio hapo Septemba 22 baada kudumu kwa Miezi 6 akiongoza Mechi 13 tu.

Inaaminika Poyet ameshafanya mazungumzo na Mmiliki wa Sunderland, Ellis Short, na anakaribia kusaini dili ya Miaka mitatu.

Poyet, mwenye Miaka 45, alitimuliwa na Brighton Mwezi Juni baada ya kuwa nao kwa Miaka minne.

Poyet, ambae ni Mtu wa Uruguay na ambae hajawahi kufundisha Klabu ya Ligi Kuu England, aliingoza Brighton kutwaa Ubingwa wa Ligi 1 Msimu wa 2010/11 ikiwa ni Miezi 17 baada ya kushika wadhifa wa Meneja na Msimu uliopita aliifikisha Timu hiyo kwenye Nusu Fainali ya Mechi za Mchujo za Daraja la Championship za kuwania kupanda Daraja kuingia Ligi Kuu lakini wakatolewa na Crystal Palace.

Mwezi Mei, Poyet, aliewahi kuwa Mchezaji wa Klabu za Grenoble, River Plate [Uruguay], Real Zaragoza, Chelsea na Tottenhma, alisimamishwa hapo Brighton kwa uchunguzi wa utovu wa nidhamu na kisha kufukuzwa Mwezi Juni.

Mpaka sasa haijulikani nini kilitokea huko Brighton hadi akafukuzwa na mwenyewe Poyet amesema atachukua hatua za Kisheria.

Akiteuliwa kuwa Meneja wa Sunderland, Poyet atakuwa Meneja wa sita wa Klabu hiyo katika Miaka mitano iliyopita.

NAHODHA MANCHESTER CITY VINCENT KOMPANY NJE WIKI 4

Vincent Kompany, Nahodha wa Manchester City na Mchezaji wa Belgium, atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki hadi 4 baada ya kuumia Nyonga kwenye Mechi ya Wikiendi City walipoifunga Everton Bao 3-1.

Hili ni pigo kwa Belgium ambao Ijumaa wanacheza Mechi muhimu ya Kundi lao dhidi ya Croatia kuwania kufuzu kwenda Brazil Mwakani kwenye Fainali za Kombe la Dunia.

Pia, maumivu hayo yatamfanya akose Mechi muhimu za Man City ambako yeye ndio nguzo kubwa kwenye Difensi na Mechi hizo ni za Ligi dhidi ya West Ham, Chelsea na Newcastle, na ile ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Ugenini huko Urusi watakapocheza na CSKA Moscow.

Siku zote kukosekana kwa Kompany, mwenye Miaka 27, ni pengo kubwa kwa City kama ilivyokuwa kwenye Mechi na Cardiff City mapema Msimu huu na City kufungwa na Cardiff bila kutarajiwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment