Klabu ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wamezuiliwa
kufanya mazoezi katika uwanja wa Taifa uliopo Jijini Dar es Salaam leo
(Alhamisi) asubuhi na kulazimika kuenda kufanya uwanja wa Polisi.
Hayo
amethibitisha na taarifa zilizotolewa na Afisa Habari wa timu hiyo
Dismas Ten wakati alipokuwa anazungumza na mwandishi wa habari hii ya
kutaka kujua sababu kubwa ya wao kuzuiliwa.
"Ni kweli tumezuiliwa kufanya mazoezi asubuhi ya leo kama
nilivyotoa taarifa katika ukurasa wetu wa timu na meneja wa uwanja
Nsajigwa Gordon ambapo ametuambia ule sio uwanja wa mazoezi ila upo kwa
ajili ya mechi", amesema Dismas.
Timu ya Yanga inatarajia kushuka dimbani siku ya Jumamosi (Februari
10, 2018) kuvaana St. Louis inayotokea visiwa vya sheli sheli na katika
mashindano ya kimataifa.

0 comments :
Post a Comment