Kesi inayomkabili aliyewahi kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira nchini
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ya kuhujumu uchumi imeahirishwa mpaka
Feburuary 22, 2018 ya mwaka huu.
Chanzo cha kuahirishwa kwa kesi hiyo ni kutokana na DPP kushindwa kukamilisha kusaini hati ya mashtaka hayo.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri ambaye
anasimamia kesi hiyo ameutaka upande wa Jamhuri kuhakikisha hati hiyo
inasainiwa mpaka kufikia tarehe hiyo ili kesi iweze kuendelea
mahakakamani hapo.
Awali Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iliieleza
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wamekwisha kamilisha upelelezi wa
kesi hiyo inayowakabili viongozi hao wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF).

0 comments :
Post a Comment