Mara baada ya Timu ya KMC kufanikiwa
kupanda daraja msimu huu kushiriki Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara msimu ujao wa
2018/19, Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjanin Sitta amesema kwa kushirikiana
na uongozi wa Timu hiyo watahakikisha timu inakuwa mfano kwa taasisi nyingine
kwa kukuza vipaji.
Sitta amesema, atahakikisha
wanakuwa na Shule ya kukuza vipaji kwa vijana ili kupata wachezaji
wazuri wa Klabu na timu ya Taifa ambao wataweza kuitangaza Tanzania kupitia
Soka hapo baadaye.
Meya Sitta amesema, kwa sasa
wanaendelea kuhakikisha waiboresha zaidi timu hiyo ambapo Siku ya Jumamosi ya
Februari 10 wanatarajia kuwa na sherehe ya kukabidhi timu hiyo kwa
wananchi ambao ndio wenye timu.
Meya Sitta ameongeza kuwa mbali na
hayo, lakini kwa sasa yupo katika mazungumzo na wadau pamoja na wadhamini
mbalimbali ili kuweza kupata watu watakaoweza kuibeba timu hiyo na kuweza
kufanikisha malengo yao ya muda mrefu na muda mfupi ikiwa ni pamoja na kujenga
Uwanja wa nyumbani.
Kwa wake Kocha wa Timu hiyo Fredy
Felix Minziro amesema, katika kuhakikisha anaboresha kikosi hicho atasajili
wachezaji wachache ambao ni wazawa na hana mpango wa kusajili wachezaji wengi
au wa Kimataifa na hata kama ikitokea kuhitaji mchezaji wa kimataifa
itawalazimu kushauriana na kumuangalia zaidi.
Kocha Minziro amesema, anaamini
kikosi kilichoipandisha timu hiyo kwenda Ligi kuu ni kizuri na chenhe uwezo
hivyo haoni sababu ya kukifanyia marekebisho makubwa.

0 comments :
Post a Comment