Afisa habari wa Klabu ya Simba Haji Manara amewaonya mashabiki wa
wekundu wa Msimbazi kuacha kuwazomea mabingwa watetezi wa Ligi Kuu
Tanzania Bara, Yanga katika mchezo wa kimataifa dhidi ya St. Louis siku
ya Jumamosi.
Manara
ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari
kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Kariakoo Msimbazi, jijini Dar
es Salaam na kuwaomba mashabiki wa soka nchini kuuziunga mkono timu zao
za nyumbani Simba na Yanga kama timu zinazo wakilisha nchi na kuacha
tamaduni za kuzomeana na kuvunjana moyo.
"Natoa wito kwa washabiki wa Simba watakaoenda uwanjani kwenye mechi ya Yanga Jumamosi wasiizomee,tuzomeane kwenye ligi ya nyumbani. Sisi sote ni watanzania na tunawakilisha nchi", amesema Manara.
Kwa upande mwingine, timu ya Simba inatarajiwa kushuka dimbani siku ya Jumapili (Februari 11, 2018) kuvaana na Gendemerie Nationale katika mchezo wao wa kimataifa huku Rais wa awamu ya pili Al Haji Hassan Mwinyi kuwa mgeni rasmi wa mechi hiyo.

0 comments :
Post a Comment