FDL: MECHI 11 WIKIENDI HII!!
PATA HABARI KAMILI:
Release No. 160
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Septemba 20, 2013
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia
raundi yake ya tano kesho (Septemba 21 mwaka huu) kwa mechi huku vinara
Simba wakiwakaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga utakuwa
mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting Stars na Rhino Rangers ya
Tabora. Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons katika pambano
litakalochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Nayo Kagera Sugar itakuwa nyumbani
kwenye uwanja wake wa Kaitaba mjini Bukoba kuvaana na Ashanti United ya
Dar es Salaam katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo
kutoka Mara.
Ligi hiyo itakamilisha mzunguko wa tano
keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo Azam na Yanga
zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikikwaruzana na
Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Ruvu Shooting inayokamata nafasi ya pili
kwenye msimamo wa ligi itakuwa mgeni wa Coastal Union katika mechi
itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Wakati huo huo, Ligi Daraja la Kwanza
(FDL) inaendelea wikiendi hii kwa mechi kumi na moja. Kundi A kesho
(Septemba 21 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Transit Camp na Green
Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam), Tessema na African Lyon
(Uwanja wa Mabatini, Mlandizi).
Ndanda itacheza na Villa Squad kwenye
Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati keshokutwa (Septembe 22 mwaka huu)
kutakuwa na mechi kati ya Polisi Dar es Salaam na Friends Rangers
katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi B kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni
Mkamba Rangers dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa CCM Mkamba, na
Mlale JKT itakuwa mwenyeji wa Kurugenzi Mafinga kwenye Uwanja wa
Majimaji mjini Songea. Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) ni Majimaji na
Kimondo katika Uwanja wa Majimaji.
Mechi za kundi C kesho (Septemba 21
mwaka huu) ni Pamba dhidi ya Polisi Dodoma (Uwanja wa CCM Kirumba,
Mwanza), Stand United na Polisi Tabora (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga)
na Kanembwa JKT itacheza na Mwadui kwenye Uwanja wa Kawawa ulioko Ujiji.
Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) Polisi Mara na Toto Africans
zitacheza Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

0 comments :
Post a Comment