Uongozi wa Ruvu Shooting umesema
ubunifu wa mbinu mpya za kuboresha kikosi chao unaofanywa na benchi zima la
ufundi ndio unaosaidia timu kuwa bora zaidi katika michezo ya Ligi kuu
uliombele yao.
Afisa habari wa Ruvu Shooting Masau
Bwire, amesema licha ya mbinu za Makocha lakini wachezaji pia wapo makini
katika kuzingatia kile wanachofundishwa ambapo ndiyo sababu ya jana kuibuka na
ushindi dhidi ya Kagera Sugar na ameongeza kuwa kwa sasa hakuna kulala kwani
mawazo na akili zote wameelekeza katika mchezo unaofuata.
"Kila kunapokucha benchi lote
la ufundi kwa kushirikiana na makocha huwa wanabuni mbinu mpya za kuiboresha
Ruvu Shooting, wanajitahidi kucheza na mapungufu waliyoyaona kupitia mchezo
uliopita na hatimaye kuiweka timu katika ubora zaidi kwa lengo la kufanya
vizuri katika mchezo unaokuja, " amesema.
Masau amesema, ushindi dhidi ya
Kagera Sugar hauwafanyi kujisahau kwani Ligi ya sasa haiitaji kulala bali
wanapaswa kupambana ili kutafuta namna bora zaidi ya kutafuta matokeo mazuri.
Masau amesema mchezo wanaoutazama
kwa sasa ni dhidi ya Lipuli FC mwishoni mwa wiki hii utakaopigwa Uwanja wa
Mabatini Mkoani Pwani hivyo wapo katika maandalizi mazuri kutokana na nguvu ya
ushindani waliyonayo wapinzani wao.
"Mechi yetu tunayoitazama kwa
sasa ni mechi ya Jumapili hii ambapo tunakwenda kupambana na Lipuli kutoka
Iringa katika Uwanja wetu wa nyumbani, wapinzani wetu sio wakubezwa kwani
ukiangalia mechi zake zilizopita unaona kabisa hali ya ushindani wanayoionyesha
hivyo Kocha anaendelea kukifua kikosi ili kuhakikisha kinafanya vizuri zaidi
mwishoni mwa wiki hii, " amesema.
Katika suala la ushindani uliopo
ndani ya Ligi Masau amesema uwiano wa pointi unazidi kumpa mashaka lakini licha
ya nafasi waliyopo hajaacha kuitabiria nafasi watakayobaki nayo mpaka hitimisho
la msimu huu.
"Hali ya ushindani kwakweli ni
mgumu Sana na sijawahi kuona ushindani ya namna hii kwani hata anayeongoza Ligi
hapishani sana na wa chini yake na hata anayeburuza mkia pia hapishani sana na
anaofuatana nao, hili linanipa wasiwasi sana lakini naamini tutamaliza Ligi
tukiwa katika msimamo mzuri na nimejitabiria mwenyewe kuwa tutamaliza tukiwa si
zaidi ya nafasi ya tano Kwenye Ligi, " amesema.

0 comments :
Post a Comment