Riyad Mahrez anatarajiwa kurejea mazoezini hii leo siku ya Ijumaa ikiwa
ni maamuzi yake binafsi na tayari kuisaidia Leicester City itakapo shuka
dimbani kuivaa Manchester City siku ya Jumamosi.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria hajafanya mazoezi na klabu hiyo
tangu kufeli kwa uhamisho wake wa kujiunga na City wakati wa dirisha la
usajili la mwezi Januari.
Meneja wa Leicester Claude Puel kupitia mkutano wake na waandishi wa
habari hapo jana siku ya Alhamisi amesema kuwa Mahrez huwenda akaukosa
mchezo huo ingawa bado haija fahamika rasmi.

0 comments :
Post a Comment