Mchezaji Robin van Persie hapo jana alifanikiwa kufunga goli lake la
kwanza tangu ajiunge na klabu ya Feyenoord na kuisaidia timu hiyo
kuchomoza na ushindi wa magoli 3 – 0 dhidi ya FC Groningen.
Van Persie ambaye amesajiliwa mwezi Januari tangu aondoke ndani ya
klabu hiyo mwaka 2004 alipo jiunga na Arsenal alifanikiwa kufunga bao
hilo dakika ya 78 akitokea benchi.
Picha za Van Persie akionekana kushangiria bao lake akiwa na wachezaji wenzake.




0 comments :
Post a Comment